Jumatano, 27 Novemba 2013

UNITED YATINGA 16 BORA KWA KISHINDO


Mabingwa wa England, Manchester United, usiku wa jana walitinga kwa kishindo kikubwa raundi ya mtoano ya timu 16 ya UCL baada ya kuitwanga timu inayokamata nasasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya Bundesliga, Bayer Leverkusen kwa bao 5-0 tena wakiwa uwani kwao huko Ujerumani.
Bao za Man United zilifungwa na Antonio Valencia, Dakika ya 22, Spahic, alijifunga mwenyewe Dakika ya 30, Jonny Evans, 65, Chris Smalling, 77, na Nani, Dakika ya 88.

Wakiwa hawafunguki kwao na Msimu huu wameshinda michezo yote waliyocheza kiwanjani hapo ukiachilia mbali suluhu waliyotoka na Mabingwa wa Germany, Bayern Munich.
Bayer Leverkusen, walipewa nafasi kubwa lakini walijikuta wako hoi bin taaban na sasa wamepitwa kwenye Msimamo wa Kundi hili na Shakhtar Donetsk ambayo nao jana waliifunga Real Sociedad Bao 4-0.
Kwenye Mechi hii, Man United walivaa utepe Mweusi mkononi kuomboleza Kifo cha Lejendari Nahodha wao, Bill Foulkes, aliefariki Wiki hii akiwa na Miaka 81, ambae alichezea Klabu hiyo Mechi 688 ambazo zimepitwa tu na Sir Bobby Charlton, Ryan Giggs na Paul Scholes.

VIKOSI:
BAYER LEVERKUSEN: Leno, Donati, Spahic, Toprak, Can, Bender, Reinartz, Rolfes, Castro, Kiessling, Son
Akiba: Lomb, Stafylidis, Wollscheid, Derdiyok, Hegeler, Kruse, Kohr.
MAN UNITED De Gea, Smalling, Ferdinand, Evans, Evra, Giggs, Jones, Valencia, Nani, Kagawa, Rooney
Akiba: Lindegaard, Anderson, Hernandez, Young, Welbeck, Cleverley, Buttner.
Refa: Svein Oddvar Moen (Norway)

KAMA ULIANGALIA MECHI GONGA LIKE, TOA MAONI YAKO
13Like ·

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni