Chelsea
wametinga raundi ya mtoano ya timu 16 ya UCL, UEFA Champions Leuague,
licha ya kufungwa bao 1-0 na FC Basel hapo jana huko Uswisi kwenye Mechi
ya Kundi E.
Nayo Barcelona, wakicheza bila ya nyota wao Lionel Messi na ambao kabla ya mechi yao ya jana walikuwa wameshatinga raundi ya mtoano ya timu 16 ya UCL, walifungwa bao 2-1 na Ajax huko Amsterdam na hicho ni kipigo cha kwa kwanza kwao msimu huu chini ya Meneja wao mpya Gerardo Martino.
Ajax sasa watasafiri kwenda Italy mwezi ujao kucheza na AC Milan ambao jana waliitandika Celtic 3-0 huko Scotland na matokeo ya mechi hii kuamua nani ataungana na Barca.
Katika Kundi F, timu 3, Arsenal, Napoli na Borussia Dortmund, zina uwezo wa kupata nafasi mbili za kutinga raundi ya mtoano ya timu 16 baada Arsenal kuifunga Olympique Marseille 2-0 na Borussia Dortmund kuichapa Napoli 3-1.
Arsenal watamaliza ugenini na Napoli na Dortmund pia watakua ugenini kucheza na Marseille ambayo imeshaaga mashindano.
Mechi za jana za Kundi G zote zilimalizika kwa Sare ya 1-1, lakini moja kati ya Zenit St Petersburg na Porto bado zina nafasi ya kuungana na Atletico Madrid raundi ijayo.
SHARE HII NA TOA MAONI YAKO UNADHANI TIMU ZIPI ZINAUHAKIKA WA KUPITA
— with Gilbert De Classic.Nayo Barcelona, wakicheza bila ya nyota wao Lionel Messi na ambao kabla ya mechi yao ya jana walikuwa wameshatinga raundi ya mtoano ya timu 16 ya UCL, walifungwa bao 2-1 na Ajax huko Amsterdam na hicho ni kipigo cha kwa kwanza kwao msimu huu chini ya Meneja wao mpya Gerardo Martino.
Ajax sasa watasafiri kwenda Italy mwezi ujao kucheza na AC Milan ambao jana waliitandika Celtic 3-0 huko Scotland na matokeo ya mechi hii kuamua nani ataungana na Barca.
Katika Kundi F, timu 3, Arsenal, Napoli na Borussia Dortmund, zina uwezo wa kupata nafasi mbili za kutinga raundi ya mtoano ya timu 16 baada Arsenal kuifunga Olympique Marseille 2-0 na Borussia Dortmund kuichapa Napoli 3-1.
Arsenal watamaliza ugenini na Napoli na Dortmund pia watakua ugenini kucheza na Marseille ambayo imeshaaga mashindano.
Mechi za jana za Kundi G zote zilimalizika kwa Sare ya 1-1, lakini moja kati ya Zenit St Petersburg na Porto bado zina nafasi ya kuungana na Atletico Madrid raundi ijayo.
SHARE HII NA TOA MAONI YAKO UNADHANI TIMU ZIPI ZINAUHAKIKA WA KUPITA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni