Mike Sangu akilia kwa uchungu baada ya kuondokewa na dada yake.
Mike alipatwa na pigo hilo wiki iliyopita baada ya dada yake huyo
kuugua kwa muda mfupi akisumbuliwa na maumivu ya titi moja lililokuwa
limevimba hali iliyosababisha kifo chake katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, Dar.“Naumia sana, dada yangu alikuwa kila kitu kwangu kwani alikuwa akinishauri mambo mbalimbali kuhusu maisha, ukweli ameniachia pengo kubwa sana ila ndiyo mipango ya Mungu nitafanyaje,” alilalama Mike kwa uchungu.
Mazishi ya dada huyo yalifanyika Ijumaa iliyopita katika Makaburi ya Kinondoni, Dar na kuhudhuriwa na watu kibao wakiwemo waigizaji wa filamu ambapo mkewe, Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ alikuwa na kibarua kizito cha kumbembeleza Mike anyamaze.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni