
Serikali imesema haitavumilia mtu au kundi la watu wa aina yoyote
ambao watabainika kuendeleza vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa
kijinsia na kutaka jamii kutumia madawati ya jinsia katika vituo vya
polisi kuripoti matukio yote ya aina hiyo ili yadhibitiwe kabla ya
kuleta madhara makubwa ikiwemo watu kupoteza maisha.
Hayo yamesemwa na waziri wa mambo ya ndani Mh Dk
Emanueli Nchimbi wakati wa uzinduzi wa dawati la jinsia pamoja na
mpango kazi wa miaka mitatu unaaonyesha majukumu ya jeshi la polisi
katika kuimaraisha mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Naye mkuu wa jeshi la polosi nchini IGP Saidi Mwema
amesema tangu kuanza kufanyiwa majaribio mpango huo umeonyesha
mafanikio makubwa na hivyo ameitaka jamii kujitokeza na kutumia dawati
hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni