KUNA
mengi ya kushangaza duniani lakini hili la kijana Hamad Issa (32)
kunaswa faragha na bibi kizee Adela Mkalau (80) linaongeza rekodi ya
mambo yanayoshangaza, Risasi Mchanganyiko lina kila kitu.
Tukio hilo la kustaajabisha limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita,
nyumbani kwa bibi huyo, Yombo –Buza, jijini Dar es Salaam ambapo wajukuu
wa bibi huyo ndiyo waliomnasa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wajukuu wa bibi huyo walifedheheshwa na
kitendo hicho hivyo kuwawekea mtego na kuwanasa kisha kumfikisha Hamad
katika Kituo cha Polisi Chang’ombe kwa tuhuma za ubakaji.
BIBI: SIJABAKWA
Katika kutafuta uhakika wa madai
ya wajukuu hao, polisi wa Chang’ombe waliagiza bibi yao aitwe ili
athibitishe madai hayo wakati upelelezi mwingine ukiendelea.
Sosi
wetu alisema kuwa bibi aliwaacha hoi polisi baada ya kufika kituoni hapo
na kukataa maelezo ya wajukuu zake, huku akisisitiza hakubakwa bali
walikubaliana na Hamad.
Baada ya bibi huyo kuondoa utata, polisi walikubali kumuachia Hamad
kisha wajukuu wakafunguliwa kesi ya kushambulia na kudhuru mwili
iliyoandikishwa kituoni hapo kwa jalada namba CHA/RB/10629/2013.
BIBI NA PAPARAZI WETU
paparazi wetu alifunga
safari hadi nyumbani kwa bibi huyo na kuzungumza naye kuhusu tukio hilo
ambapo alisema: “Sijabakwa na nimekasirishwa sana kwa kitendo cha
kumpiga kijana wangu. Wawe na heshima kwa babu yao. Sisi tunapendana,
kwa nini wanatuingilia?”
Alisema: “Siku hiyo Hamad wangu alikuja nyumbani kwangu tangu mapema. Nikaandaa chakula cha jioni, tukala pamoja kisha tukalala.
“Tukiwa usingizini, nikasikia mlango unagongwa. Kwenda kufungua,
wajukuu zangu wakaingia na kuanza kumpiga Hamad na fimbo na magongo,
wakisema eti amenibaka. Hamad atanibakaje? Kwani mimi ni mtoto mdogo?
“Isitoshe
wanamfahamu vizuri sana Hamad. Nipo naye mwaka mmoja na nusu sasa, leo
inakuwaje wanajifanya hawamjui? Siku hizi mambo yamebadilika. Mdogo
anaweza kumpenda mkubwa na mkubwa akampenda mdogo. Hakuna kosa.”
MSIKIE DOGO
Mwandishi wetu alikwenda nyumbani kwa
Hamad ambapo alimkuta akiwa hoi kitandani kwa majeraha ambapo alisema:
“Ni kweli bibi ni mpenzi wangu... na wale wajukuu zake wananifahamu
vizuri sana. Wamenipiga sana, eti nimembaka bibi yao. Siyo kweli. Sisi
ni wapenzi.”
Alipoulizwa anajisikiaje kuwa kwenye uhusiano na kikongwe huyo,
alijibu: “Hata mimi nashangaa sijui imekuwaje nikampenda. Nimejikuta
nipo kwenye uhusiano naye na kwa kweli tunapendana sana.”
WAJUKUU WANASEMAJE?
Mmoja wa wajukuu wa bibi
huyo, Margaret Cheba, akizungumza na gazeti hili kuhusu tukio hilo
alisema bibi yao amewadhalilisha sana na wanaona aibu kupita mitaani kwa
kitendo cha kutembea na Hamad.
“Hili jambo limetufedhehesha sana sisi wajukuu zake halafu hata
kimila ni tatizo, hairuhusiwi kabisa. Mbaya zaidi, bibi yetu ni mgonjwa.
Anasumbuliwa na moyo... sio wa kufanya kitendo kama kile kabisa na sisi
ndiyo tunamsaidia lakini inashangaza polisi wametubadilikia kabisa,”
alisema Cheba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni