Jumatano, 27 Novemba 2013

CECAFA || ZANZIBAR YAANZA VEMA, KENYA SULUHU


CHALENJI CUP, leo yameanza huko Nairobi, Kenya kwa Mechi mbili za Kundi A ambapo Zanzibar ilianza vyema kwa kuifunga South Sudan Bao 2-1 na Wenyeji Kenya kutoka Sare 0-0 na Ethiopia.
Mechi zote hizo zilichezwa Uwanja wa Nyayo Jijini Nairobi na ilitangulia ile ya Zanzibar na South Sudan ambapo Zanzibar waliifunga South Sudan 2-1.
Mabao ya Zanzibar yalifungwa na kiungo wa Coastal Union ya Tanga, Suleiman Kassim ‘Selembe’ katika Dakika ya 5 na Adeyoum Saleh Ahmed kwenye Dakika ya 65.
Bao la Sudan Kusini lilifungwa na Fabiano Lako katika Dakika ya 67.
VIKOSI:
Zanzibar: Abdallah Rashid, Salum Khamis, Waziri Salum, Shaffi Hassan, Mohamed Fakhi, Sabri Ali, Masoud Ali, Suleiman Kassim, Awadh Juma, Amour Omar, Khamis Mcha
South Sudan: Juma Jinaro, Atar Thomas, Philip Delfino, Edomon Amadeo, Richard Justin, Wiiam Offiri, Jimmy Erasto, Thomas Jacob, Godfrey Peter, Francis Khamis, James Joseph.

SHARE HII NA TOA MAONI YAKO

6Like ·

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni